GENERATION OF LOVE UNIT

GENERATION OF LOVE UNIT
GENERATION OF LOVE@2013

Saturday, January 25, 2014

Angalia hapa Matokeo yote na Takwimu Ligi kuu ya Vodacom michezo ya jana. Bonya hapa kujua zaidi,,, Ahsante

Yanga, Azam, City zatakata

 
Kipa wa Yanga, Deogratius Munishi akiokoa hatari kwenye lango lake, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, kwenye Uwanja wa Taifa jana.Yanga ilishinda 2-1. Picha na Michael 
Na Waandishi Wetu, Mwananchi

  • Ligi Kuu tangu ilipoanzishwa mwaka 1965 ni timu nane tu ndizo zimetwaa taji hilo huku Yanga ikiwa imechukua mara 24

Dar es Salaam.
 Mabingwa watetezi Ligi Kuu, Yanga na Azam, Mbeya City wameendeleza mbio zao kileleni mwa ligi baada ya kushinda mechi zao za jana dhidi ya Ashanti United, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar.
Yanga waliamka katika kipindi cha pili na kuichapa Ashanti kwa mabao 2-1, magoli yaliyofungwa na Didier Kavumbagu na David Luhende huku Bright Obinna akifunga bao pekee kwa wenyeji.
Kwa ushindi huo Yanga wamendelea kuongoza ligi kwa pointi 31, wakifutiwa na Azam na Mbeya City zenye pointi 30, baada ya kuzifunga Mtibwa Sugar na Kagera Sugar kwa bao 1-0.
Kocha wa Yanga, Hans Vans Pluijm alisema ilikuwa mechi ngumu na wapinzani wake walicheza vizuri.
“Pamoja na kushinda hatukucheza vizuri, ladha inatokana na hali ya hewa wachezaji walipata tabu kuhema.
“Uturuki kulikuwa joto nyuzi sita au 17, huku joto kali, walishindwa kucheza kitimu ni jambo nitakalolifanyia kazi. Nimefurahi kwa kupata ushindi huu.”
Yanga waliuanza mchezo wao taratibu na kuiruhusu Ashanti United kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo hali iliyofanya mashabiki wake kutoamini kilichokuwa kinatokea.
Kocha Mdachi, alilazimika kumtoa Said Bahanuzi na kumwingiza Simon Msuva dakika 35 kipindi cha kwanza mabadiliko yaliyozaa matunda kwani dakika 51, Yanga ilipata bao la kuongoza kupitia Kavumbagu aliyemalizia vizuri pasi ya Msuva.
Dakika tisa baadaye Ashanti walisawazisha bao hilo kupitia Obinna aliyemalizia kwa ufundi krosi ya Hussen Sued aliyekimbia na mpira kutoka winga ya kushoto na kupiga krosi kwa mfungaji.
Luhende alihakikishia Yanga pointi tatu muhimu dakika 79, baada ya kuwatoka mabeki wa Ashanti kwa kasi na kupiga shuti la pembeni lililomshinda kipa wa Daud Mwasongwe na kuingia wavuni.
Kocha wa Ashanti, Abdallah Kibadeni alisema amekubali matokeo, lakini wachezaji wake walishindwa kutumia nafasi walizopata kipindi cha kwanza huku akimshutumu mwamuzi Abdallah Hashimu kwa kushindwa kumudu mchezo huo.
Chamazi, wenyeji Azam waliutumia vizuri uwanja wao Azam Complex na kufanikiwa kushinda kwa bao 1-0, kupitia Kipre Tchetche aliyeunganisha vizuri kazi ya Joseph Kamwaga

Wenger, amshambulia Jose Morinho juu ya usajili wa Mohamed Salah kuchukua mikoba ya Juan Mata. Bonya hapa kujua zaidi


 Green light: The Reds look set to bid for Mohamed Salah

London, England.
 Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ameendelea kufanya mabadiliko katika kikosi chake baada ya juzi kumsajili winga Mohamed Salah kutoka klabu ya Basel.
Taarifa ya klabu ya Chelsea ilisema, “Klabu ya Chelsea inaweza kuthibitisha kwamba tumekubaliana na klabu ya FC Basel na tutamchukua kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mohamed Salah.”
Kutokana na makubaliano hayo, klabu ya Chelsea inatarajiwa kumtambulisha Salah siku ya Jumapili wakati Chelsea itakapokuwa ikicheza na Stoke mechi ya Kombe la FA raundi ya nne.
Salah atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Chelsea katika kipindi hiki kwani tayari imewasajili wachezaji Betrand Traore na Nemanja Matic. Wachezaji hao wamesajiliwa na Chelsea baada ya kuwauza nyota Kevin De Bruyne na Juan Mata.
Mourinho amemsajili Salah kwa sababu anaona ni mchezaji mbadala anayeweza kuziba pengo la Mata aliyeuzwa katika klabu ya Manchetser United.
Hata hivyo, usajili huo wa Mata kwenda Manchester United umeonekana kumshangaza sana kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kwani alisema Chelsea haitaathirika kwa kumuuza Mata ila timu nyingine ndiyo zitaathirika.
Wenger alisema Chelsea wameishacheza na Manchester United nyumbani na ugenini msimu huu kwa hiyo hawataathirika kwa kumuuza Mata.
“Mimi nadhani kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo kingesimamishwa wakati timu zikiwa zimeishakutana mara moja na kumalizika mzunguko wa kwanza,”alisema Wenger.
Kocha Wenger alikanusha taarifa zilizopo kwamba anataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Cristian Tello kwani alikwenda Hispania kushuhudia mechi kati ya Barcelona dhidi ya Levante.
Hata hivyo, zipo taarifa kwamba Arsenal bado inaendelea na harakati zake za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Schalke, Julian Draxler kwa ajili ya kuziba pengo la mshambuliaji wake Theo Walcott aliyeumia goti.

Mata atua rasmi Jijini Manchester kufanyiwa vipimo vya afya... Bonya hapa kuona picha yake akiwa na David Moyes.

Add captionfc nx

Wednesday, January 22, 2014

TFF YAZUIA USAJILI WA EMMANUEL OKWI YANGA, HAKUNA KUONEKANA UWANJANI MPAKA KIELEWEKE,,, bonya hapa kujua


USAJILI WA OKWI YANGA WAZUIWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana leo (Januari 22 mwaka huu) kupitia masuala mbalimbali, imesimamisha usajili huo baada ya kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.
Okwi ambaye aliingia mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile du Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.
Katika FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.
Hivyo, TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.
MECHI ZA TANZANIA PRISONS YAZASOGEZWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesogeza mbele mechi za raundi ya 14 na 15 zinazoihusu timu ya Tanzania Prisons zilizokuwa zichezwe Januari 25 na 29 mwaka huu.
Awali Tanzania Prisons ilitakiwa kutafuta uwanja mwingine wa kuchezea mechi hizo dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Ruvu kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kutokuwa tayari kwa Ligi Kuu ya Vodacom wikiendi hii.
Mechi hizo sasa zitachezwa kati ya Februari 6 na 8 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Sokoine.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Mata atua Manchester United kwa pauni milioni 37. Masaa machache baada ya kulala kwa Sunderland, Bonya hapa kujua zaidi



Juan Mata
Ombi la Manchster United la kutaka kumsajili nyota wa Chelsea Juan Matata imekubalika.
Ripoti zinasema United imetumia takriban kitita cha pauni milioni 37 kumsajili mcheza kiungo huyo wa Chelsea.
Mata mwenye umri wa miaka 25, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu baadaye hii leo, kabla ya kukamilisha usajili huo.
Mchezaji huyo kutoka Uhispania anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na nusu na klabu hiyo iliyo na makao yake katika uwanja wa Old Trafford.
Mata ambaye aliichezea Chelsea, mechi 32, aliwaaga wachezaji wenzake na wakufunzi wa Chelsea katika uwanja wao wa mazoezi wa Cobham siku ya Jumatano.

Manchester United yakana fununu


Kocha wa Manchester United David Moyes
Awali kulikuwa na fununu kuwa Mata mwenye umri wa miaka ishirini na mitano, alitaka kuondoka kutoka Chelsea, baada ya kushinda kupata nafasi miongoni mwa wachezaji wa kwanza kumi na mmoja wa Chelsea, chini ya kocha wao mpya Jose Mourinho.
Siku ya Jumanne, Chelsea ilitangaza kuwa hawana nia yoyote ya kumuuza nyota wake Mata, ambaye aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa klabu hiyo mwaka uliopita.
Lakini mchezaji huyo ambaye alikuwa kikosi cha Uhispania kilichoshinda kombe la dunia mwaka wa 2012, aliondolewa katika mechi tisa kati ya kumi na tatu alizocheza za ligi kuu ya premier msimu huu, hali iliyozua fununu kuwa huenda akauzwa mwezi huu wa Januari.
Kwingineko klabu ya Cardif inatarajia kumsaini mchezaji wa Manchester United Wilfred Saha kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.
Zaha mwenye umri wa miaka ishirini na moja alifanyiwa uchunguzi wa matibabu siku ya Jumatano na Cardiff inataka kukamilisha usajili huo kabla ya mechi yao ya raundi ya nne ya kuwania kombe la FA dhidi ya Bolton.

Tazama hapa picha iliyowekwa na Mpenzi wa Bilionea Abromovich ikionyesha uzalilishaji kwa Waafrika, Bonya hapa

Hii ndiyo picha aliyotupia katika mtandao mpenzi wa tajiri wa klabu ya chelsea Abromovich ikidaiwa kuonyesha ishala ya ubaguzi kwa Waafrika.

Saturday, January 18, 2014

Ancelot, Bacelona na A, Madrid mnipishe hapo juu nakuja kuchukua kilicho nitoa Ufaransa, Soma hapa kujua zaidi

 Real Madrid boss Ancelotti: My a*** is earthquake-proof  Kocha za Real Madrid Callo Ancelot ametoa mkwala kwa Bacelona na Jilani zao Atretic Madrid kuwa sasa timu yake inakuja kileleni mwaligi ya Laliga baada ya kufanikiwa kuibika na ushindi mnono wa mabao 5 kwa bila hapo jana usiku magoli yakitiwa  kambani na C.Ronaldo dk 10, Gareth Bale dk 25, Karim Benze
mq dk 45 , Anger dimaria dk 62, na lile la mwisho lililo fungwa na Morata dk 90,  kocha huyo mwenye mafanikio makubwa ya kushinda makombe ya ligi tatu kubwa tofauti ikiwemo Ligi ya England, Italia na Ufaransa anashika nafasi ya tatu hivi sasa akiwa nyuma ya Bacelona na A, Madrid

‘Muuaji’ wa Dk Mvungi apandishwa kizimbani..Bofya hapa kufaham zaidi


Na Jonas Emmanuel

DK Sengondo Mvungi ambaye alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliuawa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake


Dar es Salaam. Mshtakiwa George Mulungu (28) mkazi wa Vingunguti amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka la kumuua kwa kukusudia aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi.
Mulungu alisomewa shtaka la mauaji ya kukusudia juzi na Wakili wa Serikali, Charles Anindo ambaye pia alimwomba Hakimu Mkazi, Geni Dudu kuwa mshtakiwa huyo Januari 30, 2014, aunganishwe na wenzake 10 wanaokabiliwa na kesi hiyo.
Hakimu Dudu alikubaliana na ombi hilo na kuiahirisha kesi hiyo hadi Januari 30, 2014 ambapo mshtakiwa huyo ataunganishwa na wenzake Chibago Magozi (32) mfanyabiashara na mkazi wa Vingunguti Machinjioni, John Mayunga (56) mfanyabiashara na mkazi wa Kiwalani na Juma Kangungu (29) mkazi wa Vingunguti.
Wengine ni aliyekuwa mlinzi wa marehemu Dk Mvungi, Longishu Losingo (29) na Masunga Makenza (40) dereva na mkazi wa Kitunda, Paulo Mdonondo (30) Mkazi wa Tabata Darajani, Mianda Mlewa (40) mkazi wa Vingunguti, Zacharia Msese (33) mkazi wa Buguruni, Msungwa Matonya (30) mkazi wa Vingunguti na Ahmad Kitabu (30) mkazi wa Mwananyamala wilayani Kinondoni na kufanya idadi ya washtakiwa hao kufikia 11.
Awali akiwasomea hati ya mashtaka washtakiwa hao, Wakili wa Serikali, Aida Kisumo alidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja Novemba 3, mwaka 2013, walifanya kosa hilo la mauaji ya kukusudia kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria na Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Kisumo alidai kuwa siku ya tukio, katika eneo la Msakuzi Kiswegere lililopo eneo la Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao kwa pamoja walimuua kwa kukusudia Dk Sengondo Mvungi ambaye ni Mjumbe wa Tume ya Katiba Mpya.

Wednesday, October 16, 2013

JANGWANI PANOGA, WAITWA WANACHAMA KUTOA UAMUZI WA MWISHO

Na. Frank Charles Gibebe
KLABU ya Yanga ya Dar es Salaam imepiga hatua katika mchakato wa kuanzisha kampuni kwa kuanza rasmi mchakato wa kupigisha kura wanachamwa wake kuunga mkono au kupinga wazo hilo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga SC, Lawrence Mwalusako amesema leo asubuhi katika Mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam kwamba wanachama watatakiwa kufika makao makuu ya klabu kupiga kura zao.
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga SC, Lawrcence Mwalusako kulia akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu. Kushoto ni Ofisa Habari wa klabu, Baraka Kizuguto.

Mwalusako alisema kwamba kwa wanachama wa mikoani wataandaliwa utaratibu maalum wa kushiriki zoezi hilo.
Katika Mkutano wa Kawaida wa Wanachama wa Yanga uliofanyika tarehe 16 Januari 2013 Mwenyekiti kwa niaba ya Kamati ya Utendaji aliwapa Wanachama wafikirie mapendekezo ya YANGA kuwa Kampuni ama kutokuwa Kampuni kisha kuyawasilisha kwa Katibu Mkuu wa klabu.
“Nachukua nafasi hii kuwaambia Wanachama wa Yanga kuwa kuanzia leo tarehe 16 Oktoba 2013 mpaka tarehe 10 Novemba 2013, kutakuwa na sanduku moja hapa klabuni kwa ajili ya kukusanya kura za maoni ya wanachama ya kuanzisha kampuni (NDIYO) au kutokuwa Kampuni (HAPANA),”alisema Mwalusako.
Mwalusako alisema kila mwanachama hai atakuwa na uhuru wa kupiga kura na atalazimika kufika na kadi yake makao makuu ya klabu, ambapo itamzuia kupiga kura mara mbili au zaidi.
Yanga SC ilianzishwa mwaka 1935 na kwa wakati wote huo imekuwa katika mfumo wa klabu, ingawa mara kadhaa kuanzia miaka ya 1990 yalifanyika majaribio ya kuigeuza kampuni bila mafanikio na kusababisha hadi migogoro mikubwa.
Chini ya Uenyekiti wa Alhaj Yussuf Mehboob Manji, aliyeingia madarakani Julai 15, mwaka jana, Yanga SC inajaribu tena kutimiza ndoto zake za kujiendesha katika mfumo mpya wa kampuni.