GENERATION OF LOVE UNIT

GENERATION OF LOVE UNIT
GENERATION OF LOVE@2013

Friday, August 2, 2013

Maajabu,, Mtazame Mama aliyejifungua ndani ya masaa 15 baada ya kujigundua ana ujauzito..Soma Hapa

Thanks kwa Kuichagua Jonstwice
Amanda Ross akiwa amembeba mwanae. Kushoto ni mumewe, Paul Dean.
Mwanamke mmoja amejifungua mtoto wake wa kwanza masaa 15 tu baada ya kujigundua alikuwa mjamzito.
Amanda Ross, mwenye miaka 41, alikuwa amekwenda kufanya manunuzi akiwa na mpenzi wake, Paul Dean ndipo ghafla akaanza kujisikia mkakamao wa tumbo.
Alikimbilia kwenye kituo kimoja cha afya cha karibu na kuonana na daktari wa kawaida.
Walimpeleka kwa mkunga ambaye alimpima - na kumweleza kwamba alikuwa na ujauzito unaokadiriwa kuwa wa miezi saba au minane.
Amanda aliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya matibabu kidogo ya tumbo lakini ilipotimu Saa 7:30 usiku alimweleza Paul anatakiwa kwenda moja kwa moja hospitali kufuatia tumbo lake kuwa linanguruma.
Paul, ambaye ana watoto wawili na wajukuu wawili kutoka kwenye ndoa yake ya kwanza, aliwasha gari na kumpeleka Amanda kwenye hospitali ya karibu.
Haraka alichekiwa na wakati huohuo akahamishiwa kwenye gari la wagonjwa kwenda kwenye kitengo cha wajawazito cha Hospitali ya South mjini Bristol.
Amanda aliwasili hapo Saa 11:30 alfajiri ambapo vipimo vikagundua mapigo ya moyo ya mtoto huyo aliyekuwa tumboni yakidunda kwa namna ya hatari.
Madaktari wakamfanyia upasuaji na mtoto wa kike Chloe akazaliwa dakika 80 baadaye akiwa mwenye afya njema.
Amanda, ambaye hakuwahi kubeba mimba kabla, aliwekwa hospitali kwa siku sita kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani kwenye ghorofa lao lenye vyumba viwili huko Yate, South Gloucestershire.
Alisema: "Mwitikio wangu wa kwanza pale waliponiambia nilikuwa mjamzito ulikuwa wa kwenda mrama.
"Nilifikiri 'Oh Mungu wangu', ningeweza kufanya hivi miaka kumi iliyopita - lakini niko katika umri wa miaka ya 40.
"Ulikuwa ni mshituko mkubwa na bado siwezi kuamini. Inaelekea kuwafanya wengine waweze kuzoea."
Paul, mwenye miaka 53, amekuwa akiishi na Amanda kwa miaka 14 na hakuna yeyote kati yao anayefanya kazi. Tayari ni baba wa Andrew, mwenye miaka 34, na binti Jessica, mwenye miaka 32.

No comments:

Post a Comment