Thanks For Choosing Jonsttwice
Add caption |
Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai amesema Uchaguzi wa Rais nchini
Zimbabwe ulikuwa ‘kichekesho kikubwa’, akituhumu udanganyifu wa kura
uliofanywa na kambi ya mpinzani wake Rais Robert Mugabe.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Bw Tsvangirai alisema
upigaji kura uliofanyika Jumatano ulikuwa ‘upuuzi na si
halali’.Waangalizi wa uchaguzi huo wengi wao wamesema karibu watu
milioni moja walizuiwa kupiga kura.
Aidha Zanu PF imenukuliwa kudai kushinda,imekanusha tuhuma hizo ikisema upigaji kura ulikuwa shwari.
Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Afrika, Rais wa zamani wa Nigeria
Olusegun Obasanjo, alisema kwenye tathimini yao ya awali kuwa upigaji
kura ulikuwa huru na haki.Makundi mengine ya waangalizi yalisifia hali
ya amani katika uchaguzi huo.
Shughuli ya kuhesabu kura ilianza usiku na Tume ya Uchaguzi ya
Zimbabwe (ZEC) imedai kutangaza matokeo ya uchaguzi huo ndani ya siku
tano.
Tayari polisi wameonya kuwa watachukua hatua dhidi ya yeyote
atakayejaribu kuvujisha habari za matokeo. Ni kinyume cha sheria
kutangaza matokeo yasiyo rasmi.
Mji wa Harare umeenea Vikosi vya ziada vya askari baadhi vikiwa na
vifaa vya kupambana na waandamanaji na yeyote atakaye vunja sheria
wakati wa kusubiri kutangazwa kwa matokeo rasmi.
No comments:
Post a Comment