GENERATION OF LOVE UNIT

GENERATION OF LOVE UNIT
GENERATION OF LOVE@2013

Monday, August 12, 2013

LUIS SUAREZ, AGOMA KUOMBA RADHI LIVERPOOL NA YUKO TAYARI KUFANYA MAZOEZI PEKE YAKE MILELE


clip_image001Kivyake: Suarez amelazimishwa kufanya mazoezi peke yake na ataendelea kufanya hivyo hadi aombe radhiclip_image001[6]Hasira: Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema Luis Suarez hataruhusiwa kujiunga na kikosi chake hadi aombe radhi
UHUSIANO wa Luis Suarez na Liverpool utaingia katika hatua nyingine wiki hii, baada ya mshambuliaji huyo kukataa kuiomba radhi klabu kwa kauli zake kwamba alikubaliana na kocha ataondoka, kulazimisha kutimkia Arsenal.
Vyanzo vya karibu na mwanasoka huyo wa Uruguay vinaamini uhusiano wake na kocha Brendan Rodgers umeharibika kutokana na kutaka kuondoka Merseysiders kipindi hiki.
Suarez anafanya mazoezi peke yake kwenye viwanja vya mazoezi vya Liverpool, Melwood, na Rodgers amesema hatamruhusu kujiunga na timu yake hadi aombe radhi kwa kauli yake ya wiki iliyopita, akiweka wazi anataka kuhamia Emirates.
Lakini kupitia Sportsmail inafahamu kwamba Suarez hataomba radhi, akiamini amesalitiwa na kocha Rodgers juu ya makubaliano waliyofikia.
Anaamini wamekiuka makubaliano ya kiungwan waliyofikia kwamba, Liverpool, isipofuzu Ligi ya Mabingwa ataruhusiwa kuondoka.
clip_image001[9]Anasotea kifaa: Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger tayari ofa zake mbili za kumnunua Luis Suarez zimepigwa chini Liverpool
Arsenal tayari imetoa ofa ya Pauni 40,000,001 kwa ajili ya kumnunua mchezaji huyo, lakini imepigwa chini

No comments:

Post a Comment