GENERATION OF LOVE UNIT

GENERATION OF LOVE UNIT
GENERATION OF LOVE@2013

Tuesday, August 13, 2013

Hivi ndivyo vitu vinavyochangia kuondoa Radha ya Mapenzi;.. bonya hapa kujua zaidi

VITU HIVI HUONDOA RADHA YA MAPENZI
Tendo la ndoa ni tendo takatifu kwa watu waliooana na linamisingi yake ambayo ikidumishwa hakila kila mmoja atalifurahia. Kuwana baadhi ya wanawake huwa wanajisikia maumivu makali baada ya kufanya tendo la ndoa huwa kama amechanjwa na wembe.
Mara nyingi hali hii husababishwa na mwanaume mwenye kucha ndefu pindi anapokuwa katika harakati za kumwandaa. Kucha hizi kama utaziingiza sehemu za siri kwa mwanamke lazima zitamchubua na kufanya ahisi maumivu wakati wa kufanya tendo.
Mikono mikavu ambayo imeota sugu huwa kama msasa ambao humuumiza mwenzako na kusababisha michubuko kwa ndani.Vile vile unapokuwa na magonjwa ya zinaa ambayo husababisha vidonda kwa ndani na kukufanya uhisi maumivu wakati wa tendo na kushindwa kulifurahia zaidi ya maumivu muda wote.
Kingine ni kikwapa watu wengi hujisahau na kujikuta hawaheshimu tendo hili hata bila kuoga yeye anaingia kazini na kujikuta akiharibu hali ya hewa kutokana na harufu kali itokanayo na jasho la kutwa nzima.
Mara nyingi unatakiwa kuwa msafi wa mwili muda wote kwa kunyoa nywele sehemu za siri, kukata kucha huku ukihakikisha mikono yako ni misafi na laini, kuangalia afya yako kila wakati na kutibu magonjwa ya zinaa yanapokutokea, pia kuoga kabla ya tendo ili kuondoa jasho la kutwa nzima. Ni vizuri kama hujaoa ili kujiepusha na maradhi ya kuambukiza utumie kondomu kwa ajili ya kujikinga.
Tujenge utamaduni wa kuheshimu tendo la ndoa ambalo maandalizi yake yanahitaji mtu kuwa msafi tena mwenye afya bora. Nina imani mtu akizingatia yote haya ataweza kufurahia tendo lake la ndoa.

No comments:

Post a Comment