KINDA la
Burkina Faso Bertrand Traore ni mmoja wa makinda waliomvutia sana kocha
wa Chelsea Jose Mourinho katika mechi za maandalizi ya msimu mpya huko
barani Asia. (HM)
Kwa sababu ya kanuni za usajili
mchezaji huyo sio mchezaji rasmi wa The Blues mpaka atakapotimiza miaka
18 mnamo tarehe 6 September, hapo ndipo anaweza kusaini mkataba wa
kuitumikia Chelsea.
Wiki hii
katika mechi ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Malaysia XI alifunga bao
zuri sana na akaongeza bao jingine katika ushindi wa 8-1 dhidi ya
Indonesia All Stars.
"Ni kijana mdogo, lakini nina uhakika
atakuja kuwa na umuhimu sana ndani ya kikosi cha Chelsea cha baadae,"
mchezaji mwenzie Gary Cahill alisema.
Traore alikuwa sehemu ya kikosi
cha Burkina Faso kilichoshiriki michuano ya kombe la mataifa huru ya
Afrika mwaka 2012 zilizofanyika Equatorial Guinea na Gabon - alicheza
katika mechi aliyotokea benchi dhidi ya Sudan katika mchezo wa makundi.
Cahill anasema Traore sio muoga na anajiamini sana akiwa mazoezini akicheza na wachezaji wakubwa wa kikosi cha kwanza.
"Ameweza kuingia vizuri kwenye timu ya wakubwa. Amezoea. Ni mapema sana
kusema yupo tayari kucheza kwenye level ya juu, itakuwa sio vizuri
akijiamini kupita kiasi." - Cahil
Traore hakuitwa na kocha Paul Put kwa ajili ya kushiriki michuano ya
kombe la mataifa huru ya Afrika mapema mwaka huu huko Afrika ya Kusini,
ambapo timu yake ilienda na kushika nafasi ya pili nyuma ya Nigeria.
Lakini amekuwemo katika kikosi cha sasa ambacho kipo katika nafasi nzuri
ya kufuzu kuingia kwenye hatua ya mtoano ya michuano ya kufuzu kombe la
dunia.
Mapema
January 2011, Traore alikaririwa akiongea na kipindi cha Fast Track cha
BBC akisema; "Nataka kucheza kwenye kikosi cha kwanza Chelsea, nataka
kucheza kwenye Champions league na timu zenye majina makubwa.
"Nataka kucheza kila mechi ya timu ya Chelsea na huko mbeleni
ningependa kuja kuwa mchezaji bora kutoka Afrika kuichezea Chelsea."
AHSANTE KWA KUICHAGUA JONSTTWICE
No comments:
Post a Comment