GENERATION OF LOVE UNIT

GENERATION OF LOVE UNIT
GENERATION OF LOVE@2013

Monday, July 29, 2013

Kaseja atimkia DRC kongo kujiunga na FC Lipopo kuwatikisa Samata na Ulimwengu. Soma hapa





                                                                        
Wawakilishi kutoka nchini Kongo katika timu ya Football Club de Lipopo wametua nchini kufanya Maongezi na Mchezaji huru pia nahodha wa timu ya Taifa Stars Juma Kaseja katika uwezekano wa kuitumikia timu yao
Akizungumza na Jonsttwice.blogspot.com, Bulanga Ismail amesema wametua Tanzania kuongea na Kaseja pamoja na Shirikisho la Soka  Tanzania (Tff) kupata uhakika juu ya mkataba wake na Simba kama kweli upo ama umemalizika ,
Ismail amesema wamemfatilia Kaseja kwa muda mrefu sasa na kuafikiana na uwezo wa Kipa huyo kipenzi cha kocha wa Taifa Stars Kim Poulsen,
Endapo dili hiyo itafanikiwa kaseja atapewa mkataba wa miaka miwili kukupiga Lipopo na kuwa mchezaji wa pili kwa misimu ya hivi karibuni kutoka Simba Kujiunga na klabu za Kongo baada ya Samata kujiunga na Tp Mazembe na Mussa Hasani Mgosi kutimkia huko FC Motema Pembe

1 comment: