Mwanamuziki mkongwe wa kizazi kipya nchini Tanzania Rehema Charamila maarufu kama Ray C aliyekuwa ameathilika na madawa ya kulevya amewashauli vijana walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevya kuachana nayo kwani ni hatari kwa afya zao na kudai kuwa ni ugonjwa kama ilivyo kansa,kisukari nk.
Ray C ameyasema hayo wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha televishen,
na kudai vijana waachane na zile fikra potofu kwamba tatizo hilo halitibiki kwani maneno hayo si ya kweli na tiba hiyo inapatikana hapahapa Tanzania katika hospitali ya Mwananyamara na Muhimbili isiyo na malipo,
"kuna watu wengi nawafahamu haina haja ya kuwataja na wengine wavaa tai kubwa hapa nchini pamoja na wasanii wa Bongo Frava na Bongo Movie ila ipo siku Mungu atawaumbua na Watajipanga hospital kuchukua tiba" Alisema Ray C
Ameongeza kuwa baada ya afya yake kurudi upya kama hapo mwanzo baada ya kupona, anaamini atawashauri vijana wengi ambao wameathirika na madawa ya kulevya wasiwe na wasiwasi watapona kama alivyopona yeye,
No comments:
Post a Comment