Siku za mwizi ni 40....
Kauli hiyo ya wahenga ilitimia Jumatatu iliyopita kufuatia msichana
Pili Baraka (21) aliyevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake hivi
karibuni kujikuta akitupwa Gereza la Segerea jijini Dar baada ya
kunaswa kwa tuhuma za ukahaba,
Mrembo huyo alifikishwa kwenye Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) na
kusomewa shitaka na mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi
mbele ya Hakimu Timothy Lyon.
Akisoma
shitaka hilo, Magodi alisema: Agosti 5, mwaka huu, saa nane usiku, Pili
alinaswa kwenye maeneo ya Manzese jijini Dar akifanya biashara ya
ukahaba.
Aliposomewa shitaka lake hilo, Pili aliinamisha kichwa na kujibu kwa kifupi: Si kweli.
Licha
ya kukana shitaka hilo, Hakimu Lyon alimtaka mchumba huyo wa mtu
kutafuta wadhamini wawili lakini aligonga mwamba na kupelekwa Gereza la
Segerea mpaka Agosti 20, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Akijitetea
kabla ya kupandishwa kwenye karandinga kwenda Segerea, Pili aliiomba
mahakama hiyo imuonee huruma asiende kuilia Sikukuu ya Idd, Segerea kwa
kuwa mchumba’ake yuko safarini kikazi na hakuwa na mtu mwingine wa
kumwekea dhamana, ombi ambalo lilikataliwa
No comments:
Post a Comment