Jumuiya ya watanzania ugiriki baada ya kikao cha tume maalum inapenda kutoa taarifa kamili ifuatayo:
1. Waliovamiwa ni Makamu Mwenyekiti bw. SALUM MSELEM na Mhazina bw. SAID MOHAMED SAID maarufu kwa jina la NURAMO(CHIDI) NDUGU HAWA SI WAKIMBIZI, NI WATANZANIA HALISI.
2. Mabwana hao walikuwa wanapita kwenye garden usiku wa Jumatano 01/08/2013 kuelekea makwao,wakitokea kwenye kikao muhimu ofisini . Karibu na garden hiyo kulikuwa na wezi waliokuwa wanajaribu kuvunja gari iliyokuwa imeegeshwa.Wezi hao walijishuku kama Salum kawagundua wakamfuata kwa vitisho na kuanza kumpiga. Wakati huo lilitokea kundi lao jingine la watu wasiopungua kumi wakaanza kumkimbiza Chidi ambaye alijitahidi kukimbia hadi kufika chini ya nyumba anayoishi Salum(umbali wa mita 50) huku akipiga kelele na hapo waliendelea kumpiga.Kelele za Chidi kwa bahati zilisikika na mke wa Salum ambae nae alipiga kelele za kuomba msaada zilizowafanya wakimbie na kumwacha Chidi akiwa hoi.
3. Ndugu zetu tuliwafikisha hospitali na tulitoa ripoti polisi wanaoendelea na uchunguzi ambao hadi wakati huu tunapoandika maelezo haya HAKUNA TAARIFA ZOZOTE CHANYA ZA KUWAKAMATA WAHUSIKA.
4. Uongozi wa jumuiya unashindwa kutamka kuwa wezi hawa wana uhusiano na kile kikundi maarufu kinachochukia na kuwavamia wageni.Hatuna ushahidi.Bali tuna imani kubwa walikuwa ni vibaka toka nchi jirani.
5. Tumeamua kuutaarifu ubalozi na vyombo vyote vya habari vilivyokuwa vimetumiwa taarifa za awali za tukio hili.
6. Mwisho jumuiya yetu inatangaza bila kusita:
VIONGOZI WETU HAWAKUFANYA BAYA LOLOTE LILILOSABABISHA WAVAMIWE NA KUPIGWA. TUPO PAMOJA NAO KWA HALI NA MALI.
Ahsanteni
Kny
TUME MAALUM YA JUMUIYA.
(Kayu Ligopora)
No comments:
Post a Comment