Afya ya Matumaini yaimarika na ameanza kurejea katika fani yake
BAADA
ya kutoka nchini Msumbiji akiwa hoi, msanii wa vichekesho Bongo,
Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ hatimaye amepata nguvu na ameanza
kujikongoja katika kazi ya uigizaji.
Akiongea hivi karibuni, Matumaini alisema kwa sasa anaendelea vizuri na
ameshaanza kucheza filamu mbalimbali anazoshirikishwa na wasanii wenzake
na sasa anaendesha maisha yake mwenyewe.
“Nawashukuru sana wasanii wenzangu kwani
kama siyo wao, ningerudishwa nikiwa maiti, sina cha kuwalipa ila Mungu
ndiye atakayewalipa,” alisema Matumaini.
Hata hivyo, amelaani vikali baadhi ya wasanii wanaozusha maneno ya uongo
kwamba Michael Sangu alikula fedha alizokuwa anachangisha kwa ajili
yake jambo ambalo siyo la kweli.
No comments:
Post a Comment