LUIS SUAREZ, AGOMA KUOMBA RADHI LIVERPOOL NA YUKO TAYARI KUFANYA MAZOEZI PEKE YAKE MILELE
Kivyake: Suarez amelazimishwa kufanya mazoezi peke yake na ataendelea kufanya hivyo hadi aombe radhi
Hasira: Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema Luis Suarez hataruhusiwa kujiunga na kikosi chake hadi aombe radhi
UHUSIANO
wa Luis Suarez na Liverpool utaingia katika hatua nyingine wiki hii,
baada ya mshambuliaji huyo kukataa kuiomba radhi klabu kwa kauli zake
kwamba alikubaliana na kocha ataondoka, kulazimisha kutimkia Arsenal.
Vyanzo
vya karibu na mwanasoka huyo wa Uruguay vinaamini uhusiano wake na
kocha Brendan Rodgers umeharibika kutokana na kutaka kuondoka
Merseysiders kipindi hiki.
Suarez
anafanya mazoezi peke yake kwenye viwanja vya mazoezi vya Liverpool,
Melwood, na Rodgers amesema hatamruhusu kujiunga na timu yake hadi aombe
radhi kwa kauli yake ya wiki iliyopita, akiweka wazi anataka kuhamia
Emirates.
Lakini
kupitia Sportsmail inafahamu kwamba Suarez hataomba radhi, akiamini
amesalitiwa na kocha Rodgers juu ya makubaliano waliyofikia.
Anaamini wamekiuka makubaliano ya kiungwan waliyofikia kwamba, Liverpool, isipofuzu Ligi ya Mabingwa ataruhusiwa kuondoka.
Anasotea kifaa: Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger tayari ofa zake mbili za kumnunua Luis Suarez zimepigwa chini Liverpool
Arsenal tayari imetoa ofa ya Pauni 40,000,001 kwa ajili ya kumnunua mchezaji huyo, lakini imepigwa chini
No comments:
Post a Comment