Arsenal na Munich zimefikia makubaliano juu ya bei ya kiungo huyo ambayo itakuwa euro milioni 20 kabla ya kufanya mazungumzo na mchezaji mwenyewe .
Gustavo aliambiwa wazi na kocha wa Bayern Pep Guardiola kuwa hataweza kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza hali inayomfanya atafute timu ya kwenda ambayo itamhakikishia nafasi kwenye kikosi chake .
Pamoja na Higuain Arsenal imeshuhudia ofa zake mbili za kumsajili mshambuliaji Luis Suarez zikikataliwa na Liverpool ambayo imeshikilia uamuzi wa kutomuuza mshambuliaji huyo .
Hadi sasa Arsenal imesajili mchezaji mmoja pekee ambaye ni mchezaji wa timu ya vijana ya Ufaransa Yaya Sanogo
No comments:
Post a Comment