Kundi la mziki kutoka Mkoani kigoma lenye makazi yake Jijini
Dar es salaam Leka Dutigite (Kigoma All Stars) hivi karibuni wamefanikiwa
kuanzisha Sakosi itakayo kuwa na kazi moja ya kuwasaidia wasanii katika kundi
hilo ili waweze kufanikiwa katika kazi zao,
Mmoja wa wasanii na kiongozi wa kusimamia kazi zote zawasanii
katika kundi hilo
Baba Levo ameyasema hayo katika mahojiano mafupi tuliyo fanya naye hii leo na
kukiri kuwepo kwa mchakato huo ambao Ofisi zake zitakuwa Magomeni,
Baba Levo anayetamba na kibao chake kipya cha Nyong'onyeza amesema
Leka wapo katika mikakati ya mwisho kukamilisha maandalizi ya ziara zao za
kutembelea Nchi zote Afrika mashariki na mikoa yote ya Tanzania pamoja
na Vijiji vyake.

No comments:
Post a Comment