Italia
bado imendelea kukumbwa na wimbi kubwa la ubaguzi wa rangi pale Waziri
wa Kwanza Mweusi alipotupiwa ndizi alipokuwa akihutubia katika mkutano
wa Chama.
Waziri
wa Ushirikiano ni Mwitalia wa kwanza mweudi aliyeteuliwa hivi karibuni
na amekuwa akipata taabu sana kutokana na dhana ya ubaguzi iliyojengeka
miongoni mwa raia wa Italia. Cesile Kyenge ni mzaliwa wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo ambaye amekuwa akipigania haki ya wahamiaji kupata
uraia wa kudumu wa Italia.
Muda
mfupi kabla ya tukio hilo siku ya Ijumaa, wanachama wa mrengo wa kulia
Forza Nuova waliandamana wakipinga kampeni ya Waziri Kyenge ya kutaka
kumpa uraia mtu yeyote isipokuwa aliyezaliwa katika ardhi ya Italia.
“Uhamiaji
Unaua” viliandikwa baadhi ya vipeperushi ambapo ndiyo ilikuwa kauli
mbiu ya Forza Nuova wakimaanisha kuwa mauaji mengi yaliyofanyika Italia
yalisababishwa na Wahamiaji.
Ingawa
ndizi alizokuwa akitupiwa zilimkosa, Waziri Kyenge alijibu katika
mtanda wa kijamii wa twiter “sad” huzuni kwa kutupa chakula hasa katika
wakati huu wa mgogoro wa kiuchumi.“Ujasiri wa kubadilisha hali ya mambo unatoka ndani mwa mtu” alisema waziri Kyenge.
Hata hivyo, Waziri Kyenge amekuwa akikabiliwa na matusi mara kwa mara hata kutoka kwa wanasiasa wengine. Mapema mwezi huu, Mbunge mwanamizi wa kaskazini anayepinga sheria ya uhamiaji alimtukana matusi na kumlinganisha na “orangutan” Hata hivyo aliomba msamaha baadaye
No comments:
Post a Comment