GENERATION OF LOVE UNIT

GENERATION OF LOVE UNIT
GENERATION OF LOVE@2013

Thursday, July 18, 2013

NJIA za kumteka rafiki yako kuwa mpenzi wako



Watu wengi wamekuwa kama wafungwa kutokana na kushindwa namna ya kuwaambia ukweli wa moyoni marafiki zao. Wanawapenda kwa dhati, lakini watawaanzaje? Mawazo sahihi ndiyo yanahitajika katika kuamua hili.
Kesi kama hii, haihitaji uamuzi wa papara, kwani unaweza kuharibu kila kitu. Labda kabla sijaendelea mbele nikuulize swali; Umewahi kujiuliza athari za kubadili urafiki wa kawaida kuwa wa mapenzi? Kama bado, basi ni vizuri kuzitambua ili uamuzi wako usiwe na mashaka.
Huyo ni rafiki yako, mnaheshimiana na mnapendana kwa kitambo kirefu, siku mkiwa wapenzi, maana yake mnaua ule urafiki wenu uliodumu kwa miaka mingi. Aidha, kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi ni sawa na kuhatarisha maelewano mliyokuwa mmeshayajenga.
Ieleweke kwamba kuna tofauti kubwa kati ya urafiki wa kawaida na ule wa kimapenzi. Siyo rahisi kwa marafiki wa kawaida mwanaume na mwanamke kugombana na inapotokea hivyo, basi husuluhishana kisha wakaendeleza ‘safari na muziki’, lakini hiyo ni kinyume mno na wapenzi.
Ni vizuri kutambua ukweli kuwa unapoingia katika uhusiano wa kimapenzi, kwanza lazima ukubali misuguano ya hapa na pale, kushutumiana mara kwa mara na hata kugombana ugomvi mkubwa. Lakini hayo si ndiyo mapenzi?
Hata hivyo, saikolojia inafundisha kwamba ni vizuri kuacha urafiki uendelee kuliko kuugeuza kuwa mapenzi kwa sababu pengine baadaye uadui unaweza ukatokea, lakini inashauri kuwa kama upo singo na mwenzako pia ni hivyo hivyo, halafu hisia zenu zinakubaliana, si vibaya kula kitu roho inapenda.
Saikolojia inaeleza pia kwamba inawezekana faida za kugeuza urafiki kuwa mapenzi zikawa nyingi kwa sababu mnajuana muda mrefu, ni rafiki yako mkubwa ambaye mnachangia vitu vingi. Yeye ndiye msiri wako katika mambo mengi na kila unapomhitaji anakuja.
Pamoja na hivyo, umegundua yeye ndiye chaguo lako ambalo ulilingojea kwa muda mrefu. Unapomwangalia tu, unapata mshawasha wa ajabu. Tabasamu lake linakufanya utabasamu, hivyo moyoni unakiri kumpenda, lakini huo si ndiyo mzuka wa mapenzi?
Jambo la msingi hapa ni kuzingatia upendo wako, usiogope kumwingia kwa sababu eti utampoteza jumla. Fumba macho na masikio, ruhusu hisia zako zichukue nafasi, hivyo mweleze ukweli huyo rafiki yako kuwa hakuna mwingine chini ya jua hili, anayeutesa moyo wako kama yeye.
Kumwambia peke yake ni ushindi tosha kwako kwakuwa utakuwa umeshusha mzigo mzito moyoni na zaidi ukumbuke kuwa kama ulikuwa unamwonesha tabia nzuri, basi nawe utakuwa umeshamteka kihisia, kwahiyo inawezekana kumuanza kwako ukawa umemsaidia.
Zipo gia mbili za kumwingilia rafiki yako ili awe mpenzi, lakini kubwa zaidi hapa ni kwamba ili kumteka kirahisi, ni vizuri ukaongeza ukaribu, hivyo kuwa naye pamoja kwa muda mwingi na katika sehemu mbalimbali.
Kufanya hivyo, itakusaidia uzidi kumteka na kukuona wewe ni sawa na ubavu wake. Muda ambao atakuwa mbali na wewe, atajiona kama kapungukiwa na kitu fulani mwilini ambacho ni uwepo wako. Taswira ikawa ya namna hiyo, ujue kuwa hata ukimwingizia yale mambo yetu, hawezi kupindua....ENSELEA KUTEMBELEA JONSTTWICE.BLOGSPORT.COM

No comments:

Post a Comment