Kaimu mwenyekiti wa Simba SC, Godfrey Nyange Kaburu amesema
atawania nafasi ya Uenyekiti wa klabu hiyo pindi muda wa Mwenyekiti wa
sasa utakapoisha.
Akizungumza na Jonsttwice, Kaburu amesema
anajiona mwenye sifa za kuchukua nafasi hiyo na kuingoza timu hiyo yenye
maskani yake mitaa ya Msimbazi.
Kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Mbunge wa Tabora Mjini, Mh Aden Rage,
ambae katika mkutano wake uliopita na wanachama wa timu hiyo
aliwafafanulia suala la uwanja kwa Simba ni ndoto, ingawa pia Kaburu
amegusia katika mazungumzo yake kuwa hata Azam FC uwanja wao ni wa
Bakhresa na Sio Azam FC.
Lakini ikumbukwe kuwa Azam FC ni sehemu ya Kampuni ya Bakhresa hiyo
hiyo, hivyo bado Azam FC inahitaji kujivunia suala la uwanja kama vile
mambo mengine yanayohusiana na timu.
Ikumbukwe wadau wengi waliongelea na wamekuwa wakiuliza kwanini Simba
na Yanga hazina viwanja wakati Azam FC ina kiwanja? Ukweli ni kwamba
timu zote zinahitaji mikakati mathubuti ya muda mrefu, nje ya uwanja na
ndani ya uwanja.
Huenda Kaburu akaisaidia Simba isisubiri miaka 50 kujenga uwanja kama
kwa mujibu wa kauli ya Mwenyekiti wa Sasa wa simba alivyotamka.
Muda wa Aden Rage unamalizika mwakani.
No comments:
Post a Comment