Katika kuhakikisha Arsenal inarejesha heshima katika ushiriki wakea wa ligi kuu nchini England na kombe la mabingwa barani uraya Kocha mkuu wa timu hiyo ametoa ofa nyingine ya kumnyakua mshambuliji wa Uruguay na timu ya Liverpool Luis Arbelto Suarez Saga kwakutoa kiasi cha paund milion 42 baada ya ofa yao ya pili ya £40million kukataliwa Hata hivyo hapo awali Arsenal ilitoa £35m ikakataliwa na sasa wamepanda zaidi ya £7m kuhakikisha wana mnyakua mshambuliaji huyo
Arsenal inataka kuweka rekodi ya kuchukua wachezaji wenye uwezo mkubwa baada ya hapo mwanzo kutenga €27m kwa Real Madrid ili wamchukue Mshambuliaji Gonzalo Higuain, hata hivyo kuzidiwa ujanja na Napoli ambayo imetoa kiasi cha €37m. Nakuafikiana naye.
Suarez ameonekana kuwa chaguo la kwanza la Mfaransa Wenger kuliko Higuain na Wayne Rooney ambaye anatajwa sana katika mawindo ya Jose Felix Dos santos Morinho ili aweze kujiunga na klabu ya Chelsea
Arsenal inahitaji kufanya marekebisho katika kikosi chake kama inahitaji kupigania ubingwa wa ligi kuu nchini Wingereza na Klabu bingwa Ulaya hasa kwa nafasi kuu za mshambuliaji na kiungo mkabaji ambapo Uongozi umetenga €110m kuhakikisha inafanya usajili mkubwa katika msimu huu wa usajili.
No comments:
Post a Comment