Maneno mengi yamezungumzwa
baada ya Nando kutolewa katika Jumba la Big Brother huko South afrika baada ya
kutofautiana na mshiriki mwenzake Alikem raia wa Ghana nakuacha Simanzi kubwa kwa
wafatiliaji wa Big brother, Na baada ya Nando kufika Tanzania Jonsttwice ilifanikiwa
kufanya naye mahojiano mafupi na hapa anaeleza zaidi….
Jons, Nando ni Mtu gain ?
Nando,..Nimtanzania
aliye kulia mtaani na kujijengea kuwa na ndoto ya kuwa mtu mkubwa ulimwenguni
mwenye mafanikio.
Jons,..uliwaza nini hadi kushiriki
Bigbrother ?
Nando,..Nia nilikuwa nayo toka zamani
yakushiriki sababu unatakiwa uwe na mipango mingi itakayo fanikisha utoke sehem
ulipo na kufanikiwa katika maisha hasa ukiwa kijana ikanipelekea kushiriki Big
brother msimu huu,
Jons,..Siku ya kwanza ulipo fika ndani
jumba uliwaza kufanya nini kwanza kabra yayote?
Nando,..kusoma mazingira ya lile jengo na
watu waliopo mle ndani maana kamaunavyojua jons watu walikuwa wametoka nchi 14
tofauti kwa hiyo hatujuani kabisa so cha kwanza ni kuwasoma wapinzani wako
kabra.
Jons,.. Ukiwa ndani ulionyesha uwezo wa
kusakata soka vipi kuhusu hicho kipaji?
Nando,.. Yah mpira nilicheza zamani nikiwa
hapa Tanzania mechi za mchangani na nikaumia miguu nikiwa ligi daraja la tatu
hapa Dar es salaam ikabidi nisimame kucheza hadi nilipo kwenada Amerika
nikacheza kidogo bahati mbaya nikaumia tena ndipo nilipo acha Soka kabisa.
Jons,..nikipi kilicho kutoa Big Brother ?
Nando,..Nikiwa mle ndani nilifanya vitu vikuu
vitatu ambavyo Big hakuvivumilia ikabidi anitimue, kwanza nilienda na kisu
katika Party ya Chanel, O kitu ambacho hakitakiwi ila imetokea kuwa mazoea
yangu ya kutembea nacho hata nikiwa nyumbani, Pili nikakutwa tena na mkasi na
tatu ni ugonvi na Elikem,
Jons, Nafassi ya Feza kuchukua milioni 500 unaionaje
?
Nando,..Ushindani upo ila naamini atafanya
vizuri na kuwa mshidi ila hawezi kuwa mshidi bila sisi kumpigia kura ili awe
mshindi sababu yeye watanzania ndio wameishika nafasi yake mkononi kwa hiyo
tupige kura kwa wingi dada yetu ashinde.
Jons,.. Sasa hivi umerudi nyumbani je
hizo milioni ungerudi nazo uliwaza kufanya nini?
Nando,..Kuinua Entertainment ya Tanzania hasa
mziki maana ni kweli tuna maendeleo kiasi ila wenzetu wametupiga gepu kubwa
sana kama Nigeria, na nchinyingine mimi nimekaa mle ndani nimesikia Nyimbo ya
Feza tu ikipigwa kwa wasanii wetu wa Tanzania tena siku moja rabda na za Kenya chache
ila nyingi ni za wenzetu sasa niliwaza kuja kuinua mziki wetu wa hapa Bongo.
Jons,.. Unakipi cha mwisho kwa mashabiki wako
?
Nando,.. Wasahau yaliyo tokea na kuungana
wote kumpigia kura Feza, tuamini yeye bila sisi hatashinda cha kufanya ni
kuandika Vote Feza kwenda 15456 tutume zaidi na zaidi.
No comments:
Post a Comment