Yanga, Azam, City zatakata
Kipa wa Yanga, Deogratius Munishi akiokoa hatari kwenye lango lake,
katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, kwenye Uwanja wa Taifa jana.Yanga
ilishinda 2-1. Picha na Michael
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
- Ligi Kuu tangu ilipoanzishwa mwaka 1965 ni timu nane tu ndizo zimetwaa taji hilo huku Yanga ikiwa imechukua mara 24
Dar es Salaam.
Mabingwa watetezi Ligi Kuu, Yanga na Azam, Mbeya City wameendeleza mbio zao kileleni mwa ligi baada ya kushinda mechi zao za jana dhidi ya Ashanti United, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar.
Mabingwa watetezi Ligi Kuu, Yanga na Azam, Mbeya City wameendeleza mbio zao kileleni mwa ligi baada ya kushinda mechi zao za jana dhidi ya Ashanti United, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar.
Yanga waliamka katika kipindi cha pili na kuichapa
Ashanti kwa mabao 2-1, magoli yaliyofungwa na Didier Kavumbagu na David
Luhende huku Bright Obinna akifunga bao pekee kwa wenyeji.
Kwa ushindi huo Yanga wamendelea kuongoza ligi kwa
pointi 31, wakifutiwa na Azam na Mbeya City zenye pointi 30, baada ya
kuzifunga Mtibwa Sugar na Kagera Sugar kwa bao 1-0.
Kocha wa Yanga, Hans Vans Pluijm alisema ilikuwa mechi ngumu na wapinzani wake walicheza vizuri.
“Pamoja na kushinda hatukucheza vizuri, ladha inatokana na hali ya hewa wachezaji walipata tabu kuhema.
“Uturuki kulikuwa joto nyuzi sita au 17, huku joto
kali, walishindwa kucheza kitimu ni jambo nitakalolifanyia kazi.
Nimefurahi kwa kupata ushindi huu.”
Yanga waliuanza mchezo wao taratibu na kuiruhusu
Ashanti United kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo hali iliyofanya
mashabiki wake kutoamini kilichokuwa kinatokea.
Kocha Mdachi, alilazimika kumtoa Said Bahanuzi na
kumwingiza Simon Msuva dakika 35 kipindi cha kwanza mabadiliko yaliyozaa
matunda kwani dakika 51, Yanga ilipata bao la kuongoza kupitia
Kavumbagu aliyemalizia vizuri pasi ya Msuva.
Dakika tisa baadaye Ashanti walisawazisha bao hilo
kupitia Obinna aliyemalizia kwa ufundi krosi ya Hussen Sued aliyekimbia
na mpira kutoka winga ya kushoto na kupiga krosi kwa mfungaji.
Luhende alihakikishia Yanga pointi tatu muhimu
dakika 79, baada ya kuwatoka mabeki wa Ashanti kwa kasi na kupiga shuti
la pembeni lililomshinda kipa wa Daud Mwasongwe na kuingia wavuni.
Kocha wa Ashanti, Abdallah Kibadeni alisema
amekubali matokeo, lakini wachezaji wake walishindwa kutumia nafasi
walizopata kipindi cha kwanza huku akimshutumu mwamuzi Abdallah Hashimu
kwa kushindwa kumudu mchezo huo.
Chamazi, wenyeji Azam waliutumia vizuri uwanja wao
Azam Complex na kufanikiwa kushinda kwa bao 1-0, kupitia Kipre Tchetche
aliyeunganisha vizuri kazi ya Joseph Kamwaga
No comments:
Post a Comment