GENERATION OF LOVE UNIT

GENERATION OF LOVE UNIT
GENERATION OF LOVE@2013

Friday, August 2, 2013

Mugabe anaongoza kwa matokeo ya awali Asilimia 70 kumrudisha Ikulu. Soma hapa



Masanduku ya kupigia kura
Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe yanadhihirisha chama cha Rais Robert Mugabe, ZANU-PF kinaongoza.Chama hicho tayari kimedai ushindi. Msemaji wa chama hicho Rugare Gumbo alisema chama hicho kilitarajiwa kushinda kiasi ya asilimia 70 ya kura hizo.
Lakini mpinzani wa Mugabe, Morgan Tsvangirai, amesema uchaguzi huo ni wa uongo na kusema udanganyifu uliofanyika una maana uchaguzi huo haukubaliki.
Waangalizi kutoka Umoja wa Afrika na jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika wanatarajiwa kutoa tamko rasmi hii leo kuhusu uchaguzi huo.
Mkuu wa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika alisema tathmini yake ya awali ni kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na wa haki.

No comments:

Post a Comment