Kitendo cha kutajwa kuwa ni miongoni mwa Wabunge nchini wanao jihusisha na uuzaji wa Madawa ya kulevya na kusababisha vijana wengi kutumika kama wasafirishaji wa biashara hiyo kutoka nchini hatimaye
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM,
Iddi Azzan, aliyetajwa kwenye barua inayosadikiwa kuandikwa na wafungwa
Wakitanzania waliopo Hong Kong ameamua kutembelea kwenye ofisi za jeshi
la polisi na kulitaka jeshi hilo lifanye uchunguzi dhidi ya tuhuma
zilizoelekezwa kwake, ili hatua nyingine na ikibidi sheria, vichukue
mkondo wake.Akizungumza na Jonsttwice kwanjia ya Simu Azzani alisema ameamua kufika katika kituo cha Polisi ili kujua shutuma zinazo zungumzwa juu yake
"Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainike na hatua za kisheria zifuate juu yangu," Alisema Azzan kwa njia ya simu
############# Ahsante kwa kuichagua Jonsttwice ############
No comments:
Post a Comment